• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Samatta aanza kucheza Uturuki baada ya kuhama England

  (GMT+08:00) 2020-09-28 16:28:02

  Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana ametokea benchi kipindi cha pili, timu yake mpya, Fenerbahce ikilazimishwa sare ya 0-0 na Galatasaray katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki Uwanja wa Telekom Jijini İstanbul. Samatta aliyejiunga na Fenerbahce juzi kwa mkopo wa mwaka mmoja kutoka Aston Villa ya England – aliingia uwanjani dakika ya 66 kuchukua nafasi ya Mame Baba Thiam. Samatta, mwenye umri wa miaka 27 atacheza Uturuki kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu atakapouzwa moja kwa moja kwa ada ya Pauni Milioni 5.5 kumalizia mkataba wake wa Villa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako