• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Yanga na Simba waendeleza ushindi dhidi ya wapinzani

  (GMT+08:00) 2020-09-28 16:28:27

  Yanga SC wameendeleza staili yao ya ushindi mwembamba katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya leo pia kuichapa Mtibwa Sugar 1-0 Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, beki Mghana, Lamine Moro aliyeunganisha kwa mguu wa kulia kona ya chini chini ya kiungo Muangola, Carlos Carlinhos dakika ya 61. Na kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 10, sawa na mabingwa watetezi, Simba SC. Jumamosi mabingwa watetezi, Simba SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Gwambina FC 3-0 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Simba SC inafikisha pointi 10 baada ya kucheza mechi nne, sasa ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Azam FC inayoongoza kwa pointi 12. Simba SC ilikwenda kupumzika ikiwa inaongoza 1-0 kwa bao la mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, mzaliwa wa Uganda, Meddie Kagere dakika ya 39 akimalizia pasi ya kiungo kutoka Msumbiji, Luis Miquissone.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako