• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahakama ya Marekani yatoa hukumu ya kuahirisha utekelezaji wa amri ya serikali ya kuiondoa TikTok kutoka duka la App la Marekani

    (GMT+08:00) 2020-09-28 16:46:22

    Mahakama ya Washington D.C. ya Marekani imetoa hukumu ya kuahirisha utekelezaji wa amri ya serikali ya Marekani ya kuondoa app ya TikTok kutoka kwenye duka la App la Marekani.

    TikTok imekaribisha hukumu hiyo kupitia taarifa ikieleza kuwa itaendelea na mazungumzo na serikali ya Marekani. Wizara ya biashara ya Marekani pia imetangaza kuwa itafuata hukumu hiyo na kuanza mara moja hatua zinazohusika, lakini itaendelea kulinda amri na hatua zinazohusika.

    Katika mkutano wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, wakili wa TikTok John Hall amesema marufuku yoyote juu ya upatikanaji wa TikTok kwenye duka la App ya Marekani "haijawahi kutokea hapo awali" pia "haifai", na itakuwa pigo la moja kwa moja kwa mashirika, na itaweza kuwafanya watumiaji kushindwa kupokea toleo jipya la ulinzi wa usalama mtandaoni, na hivyo kudhuru usalama, na kwamba ikiwa utekelezaji wa amri ya marufuku hiyo utaanza, basi utaleta athari mbaya sana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako