Saudi Arabia ikiwa ni mwenyekiti wa zamu wa kundi la G20 imetoa taarifa kuwa mkutano wa viongozi wa nchi za kundi hilo utafanyika tarehe 21 na 22, mwezi wa Novemba kwa njia ya video.
Taarifa imesema mkutano huo utaendeshwa na mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz Al Saud na kujadiliana kuhusu kulinda afya na kufufua uchumi.
Taarifa pia imesema kundi hilo limeshatoa msaada wa fedha wa dola za Marekani bilioni 21 katika kupima, kutibu na kutengeneza chanjo ya virusi vya Corona na kutoa dola za Marekani trilioni 11 kusaidia uchumi wa dunia, ikiwemo kutoa wito kuahirisha madeni ya nchi zilizokithiri umaskini duniani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |