• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa baraza la taifa la maafikiano la Afghanistan aenda Islamabad baada ya mazungumzo ya amani kukwama

    (GMT+08:00) 2020-09-28 17:00:46
    Mwenyekiti wa baraza la taifa la maafikiano la Afghanistan Bw. Abdullah Abdullah ameondoka Kabul kuelekea Islamabad ili kubadilishana mawazo kuhusu mambo ya maslahi ya pamoja ikiwa ni pamoja na mchakato wa kisiasa unaoendelea nchini Afghanistan.
    Kwenye ziara rasmi ya siku tatu Bw. Abdullah atakutana na waziri mkuu wa Pakistan Bw. Imran Khan, Rais Arif Alvi, Mwenyekiti wa baraza la Seneti Bw Sadiq Sanjrani, pamoja na waziri wa mambo ya nje Bw. Shah Mahmood Qureshi. Hii ni ziara ya kwanza kwa Bw. Abdullah nchini Pakistani akiwa mwenyekiti wa baraza hilo.
    Ziara hiyo inafanyika wakati kuna mkwamo kwenye mazungumzo ya pande za Afghanistan mjini Doha, ambako tangu mazungumzo yaanze Septemba 12 hakuna maendeleo yaliyopatikana.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako