• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China asema nchi kubwa haimaanisha ina haki kubwa zaidi, bali ina wajibu mkubwa

    (GMT+08:00) 2020-09-28 18:06:33

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana amezungumza na mwenyekiti wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Bw. Volkan Bozkir kwa njia ya simu.

    Bw. Wang Yi amempongeza Bw. Volkan Bozkir kushika madaraka ya mwenyekiti wa baraza kuu la 75 la Umoja wa Mataifa, na kusema huu ni mwaka wa 75 tangu Umoja wa Mataifa kuanzishwa, na awamu hii ya baraza kuu ina muhimu mkubwa.

    Bw. Wang Yi amesisitiza kuwa dunia imeingia katika zama ya kuungana na kuwasiliana, hali ya upande mmoja, hali ya kujilinda na hali ya kujitenga hazina nafasi, pia hazitaendelezwa. Nchi kubwa haimaanishi kuwa ina haki kubwa zaidi, bali ina wajibu mkubwa zaidi.

    Amesema China ikiwa mjumbe wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, itashikilia kuunga mkono mfumo wa kimataifa chini ya Umoja wa Mataifa, kuunga mkono utaratibu wa kimataifa juu ya msingi wa sheria za kimataifa.

    Bw. Bozkir amesema kipaumbele cha kazi yake ni kusukuma mbele kutimiza lengo la ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, kujitahidi kuondoa umaskini na kuzisaidia nchi zenye mahitaji hasa nchi ndogo na za ukubwa wa kati. Amesema anatarajia kushirikiana na China kuimarisha utaratibu katika kulinda hali ya pande nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako