• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UN iko tayari kuyasaidia mataifa yasiyo na bahari, kujikwamua na COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-09-28 18:30:25

    Mfumo wa umoja wa Mataifa umesema unashikamana na mataifa yanayoendelea yasiyo na bahari ambayo yanakosa fursa muhimu za viunganishi vya biashara na kuyasaidia katika juhudi zao za kujijenga upya pindi janga la corona au COVID-19 litakapokwisha.

    Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres wiki jana, akizungumza kwa njia ya video kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi hizo. Bwana Guterres amesema kwamba zaidi ya changamoto ambazo zinajumuisha uingiliaji mkubwa na uvurugaji wa biashara, usajiri na usambazaji, hatari ya changamoto ya madeni nayo inanyemelea.

    Changamoto kubwa sio tu kwamba zinatishia ukuaji wa uchumi na maisha bali pia zinaathiri uwezo wa mataifa hayo kutekeleza ajenda ya 2030 ya maendfeleo endelevu na mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi, ameongeza bwana Guterres.

    Suluhu hizo zinajumuisha upunguzaji wa hewa chafuzi, miundombinu na usafiri salama, kukusanya fedha kutoka kwa wafadhili wa serikali na binafsi kuepuka kuwa tegemezi wa uchumi unaotegemea mafuta kisukuku na kuingia katika mifumo ya nishati jadidifu na kupambana na uingizaji haramu wa fedha.

    Pamoja ya hayo ameongeza kuwa uwezekano wa biashara katika nchi zisizo na bahari lazima uongezwe na ushirikiano baina ya nchi zinazoendelea zisizo na bahari na zile wanakopitishia bidhaa zao lazima uimarishwe.

    Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema mkutano wa viongozi wa masuala ya fedha kwa ajili ya maendeleo wakati huu wa COVID-19 na zaidi utakaofanyika Jumanne ijayo utasaidia kuchagiza dhamira hiyo na hatua za kuchukuliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako