• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa Beijing kuongeza uwezo wa utalii wakati wa mapumziko ya siku ya taifa kwa tahadhari

    (GMT+08:00) 2020-09-28 19:19:39

    Mji wa Beijing utaruhusu watu zaidi kutembelea vivutio vya utalii wakati wa mapumziko ya sikukuu ya Mid-Autumn na siku ya taifa, wakati hali ya maambukizi ya COVID-19 ikiwa imetulia.

    Sehemu za vivutio zitaongeza idadi ya watu wanaoruhusiwa kuingia kutoka asilimia 50 hadi 75 ya uwezo wake katika kipindi cha siku 8 za mapumziko, sambamba na mwongozo uliotolewa mwanzoni mwa mwezi huu wa kufufua kwa kasi utalii wa ndani uliotolewa na wizara ya utamaduni na utalii ya China.

    Mji wa Beijing utaendelea kutumia utaratibu wa vivutio vya utalii kutumia mfumo wa kuagiza tiketi na kupanga muda wa kuruhusu watu kutembelea. Mapumziko ya siku ya taifa yataanza Oktoba Mosi na mwaka huu yanaingiliana na sikukuu ya Mid-Autumn na kuwa mapumziko ya siku nane.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako