• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watoto watatu na wanawake wawili wauawa kwenye shambulio la roketi karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad

    (GMT+08:00) 2020-09-29 09:11:01

    Watoto watatu na wanawake wawili wameuawa jana Jumatatu baada ya roketi mbili kuangukia kwenye nyumba yao karibu na Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Baghdad.

    Ofisi ya habari ya Kamandi ya Operesheni ya pamoja ya Iraq imesema watoto wengine wawili walijeruhiwa kwenye shambulizi la roketi huko Katyusha ambalo limeteketeza nyumba ya familia kwenye eneo la Albu-Amir kusini magharibi mwa Iraq. Taarifa imeongeza kuwa roketi hizo zilirushwa na magenge ya wahalifu na makundi haramu kutoka mtaa wa jirani wa al-Jihad.

    Waziri mkuu Mustafa al-Kadhimi ambaye pia ni jemedari mkuu wa jeshi la Iraq aliamuru kukamatwa kwa maafisa wanaoshughulikia usalama kwenye mtaa wa al-Jihad na kuchunguza haraka tukio hilo. Hadi sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako