• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wang Yi: Virusi vya kisiasa vinavyochochea uhasama na mvutano ni tishio kwa dunia

    (GMT+08:00) 2020-09-29 09:29:27

    Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi amesema virusi vya Corona ni adui wa binadamu wote, na virusi vya kisiasa vinavyochochea uhasama na mvutano pia ni tishio kwa dunia nzima.

    Wang amesema hayo kwenye ufunguzi wa kongamano la "utaratibu wa kimataifa na usimamizi wa dunia kufuatia janga la COVID-19". Amesema binadamu wanaishi katika dunia iliyo kama kijiji, na janga la COVID-19 limefanya ushirikiano wa kimataifa uhitajike zaidi. Binadamu wanapaswa kushikamana ili kushinda janga hilo. Lakini wakati huohuo watu wachache wanachochea uhasama, na kupaka matope nchi nyingine ili kuhamisha lawama kwengine.

    Aidha, Wang amesema tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, China imekuwa mlinzi thabiti wa haki za kimataifa, taratibu za pande nyingi, na sheria za kimataifa, na inafuata kanuni za kuishi pamoja kwa amani na kupinga vitendo vya umwamba na kukandamiza nchi dhaifu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako