• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapenda kuendelea na juhudi kwa ajili ya utulivu na maendeleo ya Mali

    (GMT+08:00) 2020-09-29 09:34:32

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin jana kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema, rais wa mpito wa Mali Bah Ndaw ameshaapishwa, hii ni hatua muhimu ya mchakato wa mpito nchini Mali.

    Bw. Wang amesema siku zote China inaiheshimu Mali kwa kuchagua njia yake ya maendeleo, na China inatumai kuwa pande husika nchini Mali zinaweza kuendelea na juhudi, kuhimiza mchakato wa mpito kwa utaratibu na kutimiza utulivu wa maendeleo ya taifa mapema. Vilevile amesema, ikiwa rafiki mzuri wa Mali, China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa na kufanya juhudi kwa ajili ya utulivu na maendeleo ya Mali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako