• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UM azitaka Azerbaijan na Armenia zisitishe mapambano

    (GMT+08:00) 2020-09-29 09:36:24

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana aliwataka viongozi wa Azerbaijan na Armenia wachukue hatua mara moja ya kusitisha mapigano.

    Kwa mujibu wa msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric, Bw. Guterres amefanya mazungumzo na rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan na waziri mkuu wa Armenia Bw. Nikol Pashinyan.

    Msemaji huyo amesema, Bw. Guterres amefuatilia mgogoro unaoendelea kwenye eneo la Nagorno-Karabakh, na amewataka viongozi hao wawili wachukue hatua mara moja ya kusitisha mapambano na kurejesha mazungumzo, ili kuzuia machafuko kwenye eneo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako