• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujenzi wa aina mpya ya miundombinu nchini China wahimiza uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2020-09-29 14:48:46

    Vyombo vya habari vya kigeni vimesema, kutokana na kufufuka kwa uchumi na ujenzi wa aina mpya ya miundombinu nchini China, uchumi wa dunia umekua vizuri kuliko ulivyotarajiwa.

    Gazeti la European Times limetoa ripoti ikisema, China imezindua mpango mkubwa wa ujenzi wa aina mpya ya miundombinu, ikiwa ni pamoja na hesabu ya mawingu, data kubwa, akili bandia, 5G na mtandao wa kiviwanda. Hali hii si kama tu itanufaisha soko la kimataifa la chuma, na bali pia itanufaisha uchumi wa dunia.

    Gazeti la The Wall Street limesema, ikiwa nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi, China inatumia takriban asilimia 50 ya shaba duniani, na ukuaji wa sekta ya uzalishaji nchini China umesababisha ongezeko la bei ya chuma katika soko la kimataifa.

    Gazeti la Business la Korea ya Kusini limesema, kutokana na aina jhiyo mpya ya ujenzi wa miundombinu, China inahimiza kufufuka kwa soko la chuma duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako