• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makampuni maarufu ya magari duniani yana imani kubwa na soko la China

    (GMT+08:00) 2020-09-29 18:09:05

    Maonesho ya Kimataifa ya Magari ya Beijing ya mwaka 2020 yamefunguliwa tarehe 26 Mwezi huu. Haya ni maonesho ya kwanza ya kimataifa ya magari wakati wa janga la virusi vya Corona, lakini yamevutia makampuni mengi maarufu ya kimataifa, na kufuatiliwa na vyombo vya habari vya kigeni.

    Vyombo vya habari vya kigeni vinaona wakati miji ya Ulaya inapoanzisha tena hatua za zuio, na idadi ya maambukizi imezidi milioni saba nchini Marekani, Maonesho ya Kimataifa ya Magari ya Beijing yameonesha wazi mafanikio yaliyopatikana na China katika kupambana na virusi. Shirika la habari la Marekani AP limeripoti kuwa China ni kundi muhimu la kwanza la kiuchumi duniani linalofufuka kutoka kwenye maambukizi ya COVID-19, na makampuni mbalimbali maarufu ya kimataifa ya utengenezaji wa magari yanafuatilia China.

    Bw. Jochen Goller ambaye ni ofisa mtendaji mkuu wa kampuni ya BMW nchini China, amesema Maonesho ya Kimataifa ya Magari ya Beijing ya mwaka 2020 ni alama ya matumaini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako