• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uingereza yasema itaendelea kutekeleza mswada wa sheria inayovunja sheria ya kujitoa kwa Umoja wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2020-09-29 18:24:39

    Serikali ya Uingereza imejiweka kwenye migongano na Umoja wa Ulaya baada ya kukataa mwito wa kuondoa mswada wa sheria wenye utata utakaovunja sheria ya kimataifa.

    Umoja wa Ulaya umempa waziri mkuu wa Uingereza Bw Boris Johnson hadi Jumatano kuondoa vipengele kuhusu mswada wa sheria ya soko la ndani ambao kwa sasa uko kwenye mchakato wa kujadiliwa ndani ya bunge. Umoja wa Ulaya umetishia kuchukua hatua kama Uingereza itaendelea na vipengele vinavyopingwa kwenye mswada huo.

    Mgongano huo umejitokeza kwenye kamati inayosimamia mambo ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya. Uingereza inasema vipengele vinavyokosolewa vina lengo la kulinda jamii za Ireland Kaskazini, na kusema havitaondolewa kwenye muswada huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako