• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM watoa wito kwa pande mbalimbali kutoa dola bilioni 35 za Marekani ili kuharakisha upatikanaji wa chanjo cha COVID-19

    (GMT+08:00) 2020-09-29 18:39:01

    Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bibi Amina Mohammed ametoa wito kwa pande mbalimbali kutoa zaidi ya dola bilioni 35 za Marekani kuharakisha kutimiza malengo ya uendelezaji, utengenezaji na matumizi yenye usawa ya chanjo na vifaa vya matibabu ya COVID-19.

    Bibi Mohammed amesifu kazi za mashirika ya kimataifa ya afya, taasisi, mifuko na idara za binafsi za kupambana na COVID-19. Amesema bado wanahitaji fedha hizo kutimiza utengenezaji wa chanjo bilioni 2, kutoa matibabu kwa watu milioni 245 na upimaji milioni 500.

    Pia amesema dola bilioni 15 za Marekani zitahitajika ndani ya miezi mitatu ijayo ili kuharakisha kazi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako