• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vituko kwenye soka wiki iliyopita

  (GMT+08:00) 2020-09-29 19:03:01

  Ndege aina ya Tausi anayefahamika kwa jina la Macau, aliruka na kwenda kutua kichwani kwa mchezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Brazil, wakati wachezaji hao wakifanya mazoezi katikati ya wiki iliyopita. Mmoja kati ya makocha wasaidizi wa timu hiyo alichukua mpira na kwenda kuuweka karibu na ndege hayo ambaye baadaye aliruka. Hali kama hii ilitokea nchini Uingereza ambako mnyama aina ya Alcapa aliingia uwanjani kwenye mazoezi kati timu zisizo kwenye ligi ya Carlton Athlectics na Ilkely, mnyama huyo alikaa uwanjani kwa muda wa dakika 20.

  Kwingineko nchini Estonia mchezaji alibadilishwa katika sekunde ya 13 tangu mchezo uanze katika hali iliyowashangaza wengi. Licha ya kuwa mchezaji aliyebadilisha hakuumia, hii ni kutokana na sheria za soka za nchi hiyo kuwa lazima wachezaji wawili wenyeji waanza kwenye kila mechi. Mchezaji huyo hakugusa hata mpira na akatolewa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako