• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Liverpool yaisambaratisha Arsenal kwenye premier league

  (GMT+08:00) 2020-09-29 19:03:21

  Jana michezo ya ligi kuu ya Uingereza iliendelea huku viwanja vikiwa vitupu, na jana kulikuwa na mechi kati ya Liverpool na Arsenal. Kama ilivyotarajiwa ilipata ushsindi mnono na kocha Jurgen Klopp amesema timu hiyo ina jukumu la kuendelea kushinda kila mechi ndani ya Ligi Kuu England ili kuweza kutetea taji lao. Arsenal ilianza kuwafunga Liverpool katika dakika ya 25 kupitia kwa Alexandre Lacazette, lakini goli lilidumu kwa dakika mbili pekee kwani Liverpool walisawazuisha kupitia kwa Sadio Mane katika dakika ya 28. Washambuliaji wa Arsenal wakiwa na Pierre Emerick Aubameyang walihaha kutafuta magoli na kujikita wakifungwa bao la pili dakika ya 34 na Andrew Robertson, na dakika ya 88 na Diogo Jota. Klopp amesema ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kushinda tena taji la Ligi Kuu England kazi yao ni moja kuendelea kushinda mechi zao zote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako