• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya Dunia yainua makadirio ya ongezeko la uchumi wa China kwa mwaka huu

    (GMT+08:00) 2020-09-29 19:48:34

    Benki ya Dunia tarehe 28 ilitoa ripoti ya hali ya uchumi ya Asia Mashariki na Pasifiki, ikikadiria kuwa ongezeko la uchumi wa China litafikia asilimia 2 mwaka huu, likiongezeka kwa asilimia 1 kuliko makadirio ya mwanzoni mwa mwezi Juni.

    Ripoti hiyo inakadiria kuwa uchumi wa Asia Mashariki na Pasifiki utaongezeka kwa asilimia 0.9, ambayo itakuwa kasi ya chini zaidi tangu mwaka 1967, uchumi wa makundi mengine ya kiuchumi katika eneo hilo isipokuwa China utapungua kwa asilimia 3.5.

    Mwanauchumi mwandamizi wa eneo la Asia Mashariki na Pasifiki wa Benki ya Dunia Aaditya Mattoo, amesema maambukizi ya virusi vya Corona yamesababisha watu milioni 5 wa eneo hilo warejee kwenye hali ya umaskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako