• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wilaya na vijiji vyote nchini China vyaunganishwa na huduma ya usafiri wa mabasi

    (GMT+08:00) 2020-09-29 19:49:15

    Huduma za mabasi ya abiria sasa zitakuwa zinapatikana katika wilaya na vijiji vyote nchini China kuanzia mwezi Agosti mwaka huu.

    Naibu waziri wa usafiri wa China Bw. Dai Dongchang amesema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2019, umbali wa barabara ya kasi katika maeneo ya vijijini ulifikia kilomita milioni 4.2, huku wilaya na vijiji vyote vikiwa vimeunganishwa na barabara ya lami na saruji.

    Bw. Dai amesema hii ni sehemu ya juhudi za serikali katika kupambana na umaskini kupitia miundo mbinu ya usafiri.

    Juhudi pia zimefanywa katika kuimarisha mtandao wa usambazaji wa mizigo vijijini, ambao umeweka njia kwa bidhaa za mijini kufikia maeneo ya vijijini, na kukuza uuzaji wa mazao ya kilimo katika masoko ya mijini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako