• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika imepoteza zaidi ya dola bilioni 830 kutokana na uhamishaji haramu wa fedha na mali

    (GMT+08:00) 2020-09-29 19:50:41

    Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba Afrika imepoteza zaidi ya dola bilioni 830 katika miaka 15 ya kwanza ya karne hii, ikiwa ni bidhaa na fedha zinazoenda nje ya bara hilo kwa jnjia haramu.

    Nyingi za fedha au mali zenye thamani kubwa ni kama dhahabu, almasi, na platinamu na hivyo kupunguza uwezo wa serikali za bara hilo kutoa huduma kama za afya, elimu, na miundombinu.

    Hayo yamebainishwa kwenye ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa na Biashara na Maendeleo UNCTAD kuhusu maendeleo ya uchumi barani Afrika hasa uhamishaji haramu wa kifedha, au harakati haramu za pesa na mali kuvuka mipaka.

    Ripoti hiyo imeonesha kuwa sehemu kubwa zaidi ya uhamishaji haramu kutoka Afrika ni jumla ya dola bilioni 40 mwaka wa 2015 na ilihusiana na bidhaa za uchimbaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako