• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano Mkuu wa 75 wamalizika huku viongozi wakiunga mkono utaratibu wa pande nyingi

    (GMT+08:00) 2020-09-30 08:55:54

    Mkutano mkuu wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) umefungwa jana Jumanne katika makao makuu ya UM New York huku idadi kubwa ya viongozi duniani na wawakilishi wa taifa wakionyesha mtazamo chanya na kuunga mkono kwa nguvu utaratibu wa pande nyingi na Umoja wa Mataifa.

    Akiongea kwenye ufungaji wa mkutano huo rais wa Baraza Kuu la 75 wa UM Volkan Bozkir amesema viongozi wengi wametambua kuwa utaratibu wa pande nyingi unawakilisha mfumo mzuri zaidi wa kukabiliana na changamoto duniani, kama vile janga la COVID-19 na mabadiliko ya tabia nchi.

    Aidha ameeleza matumaini yake kwamba katika mwaka ujao na miezi ya mbele, atategemea zaidi nchi wanachama wa UM na viongozi wao kumuunga mkono juu ya kuendelea kufuata utaratibu wa pande nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako