• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalamu wa China aona mchango wa China kwa ukuaji wa uchumi utadumisha asilimia 30 na zaidi

    (GMT+08:00) 2020-09-30 17:10:54

    Mshauri wa Baraza la Serikali la China, na mkuu wa heshima wa Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo ya Taifa kwenye Chuo Kikuu cha Beijing Bw. Lin Yifu, amesema mchango mkubwa wa China kwa ukuaji wa uchumi wa dunia ni kudumisha ukuaji mzuri na wa kasi wa uchumi, akiona mchango wa kila mwaka wa China kwa uchumi wa dunia utaweza kudumisha asilimia 30 na zaidi.

    Bw. Lin Yifu anaona katika mchakato wa upanuzi wa soko la ndani, China itatoa soko kubwa zaidi kwa uchumi wa kimataifa, ambao utahimiza maendeleo ya nchi nyingine duniani. Pia anaona maendeleo ya China yatachangia kusaidia dunia kupambana na uratibu wa upande mmoja na kujilinda kibiashara, na kwamba uchumi wa China ukiendelea kudumisha ongezeko la kasi, na kuendelea kufungua mlango, itahimiza nchi nyingine kuelewa vizuri faida za utandawazi, na pia kuzisaidia nchi nyingine kupata maendeleo zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako