• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FAO yataka nchi zote zikabiliane na ufujaji na upotezaji wa chakula

    (GMT+08:00) 2020-09-30 18:56:29

    Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO jana kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya mwamko kuhusu upotezaji na ufujaji wa chakula, limezikumbusha nchi zote duniani kukabiliana na kile ilichoitwa "changamoto kubwa ya wakati wetu".

    Wito huo umetolewa kwenye mkutano wa pamoja uliofanyika mjini Rome kwa njia ya video na wataalamu wa FAO, Shirika la mpango wa mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa. Ujumbe muhimu uliotolewa kwenye mkutano huo ni kuwa kila mtu, kuanzia mamlaka za umma na mashirika binafsi, academia na watu binafsi kufanya kazi zaidi ili kupunguza upotezaji na ufujaji wa chakula.

    Mkurugenzi wa FAO Bw. Qu Dongyu amesema mwamko huo unatakiwa kuanza kwenye ngazi ya chini, na katika ngazi ya familia, kuwaelimisha watoto na kuthamini chakula.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako