• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump na Biden wapambana vikali kwenye mdahalo wa uchaguzi mkuu

    (GMT+08:00) 2020-09-30 18:57:01

    Rais Donald Trump wa Marekani na mgombea urais kupitia chama cha Democrat Bw. Joe Biden, leo wamepambana vikali kwenye mdahalo wa kwanza kwa ajili ya uchaguzi wa rais wa nchi hiyo.

    Mwendesha mdahalo huo ambaye ni mtangazaji wa Televisheni ya Fox News ya Marekani Bw. Chris Wallace alianza kwa kumuuliza Bw. Trump kuhusu uteuzi wa jaji wa mahakama kuu wa Bibi Amy Barrett, lakini Trump alijibu kwa kusema sasa wanadhibiti seneti, Ikulu na tayari wana mteule mzuri kwa kila njia. Bw. Biden amesema licha ya kuwa Bibi Barrett ni jaji mzuri, tayari uchaguzi umeanza na mchakato huo ulitakiwa kusubiri uchaguzi umalizike.

    Wagombea hao wawili pia wamegongana kwenye suala la bima ya afya inayofahamika kwa jina la Obamacare ambayo Rais Trump ameshindwa kuiondoa, na Bw. Biden amesema uteuzi wa Jaji Barrett una lengo la kuondoa bima hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako