• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chanjo ya China itakuwa bidhaa ya umma duniani na bei yake itakuwa ya chini

    (GMT+08:00) 2020-09-30 19:09:47

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin, amesema ili kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona, China inaharakisha kuhimiza uzalishaji wa chanjo.

    Hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari vinasema bei ya chanjo ya Corona ya China itakuwa na gharama ya juu kuliko zile za Ulaya na Marekani. Bw. Wang Wenbin amesema China imetangaza chanjo ya Corona itakuwa bidhaa ya umma ya dunia nzima baada ya kutumika, ili kutoa mchango kwa ajili ya kupatikana na kumudu katika nchi zinazoendelea, na ahadi ya China ni dhahiri, hakika itatimizwa.

    Amesisitiza kuwa hivi sasa chanjo za nchi mbalimbali ziko katika mchakato wa utafiti, bado kuna hali ya kutohakikishwa kuhusu bei. Kwa upande wa China, hakika itaifanya chanjo yake kuwa bidhaa ya umma kwa dunia nzima kwa bei nafuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako