• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Lampard asema wachezaji wake wamefungwa na Tottenham kutokana na uchovu

  (GMT+08:00) 2020-09-30 19:17:06

  Kocha Mkuu wa Chelsea Frank Lampard, amesema kupoteza kwake mechi mbele ya Tottenham Hotspurs kumemvuruga kwa kuwa walianza kushinda ndani ya dakika 45 za mwanzo. Mchezo huo wa Kombe la Carabao hatua ya 16 bora uliochezwa usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa nyumbani wa Tottenham Hotspur ulikuwa na ushindani mkubwa na dakika 90 zilikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 jambo lililopelekea mshindi kupatikana kwa penalti. Timo Werner ndio alianza kufunga goli katika dakika ya 19 alianza kufunga kwa Chelsea na lilisawazishwa dakika ya 83 na Erik Lamela ambapo kwenye penalti, Spurs inayonolewa na Jose Mourinho ilishinda penalti 5-4.Mason Mount alikosa penalti kwa upande wa Chelsea. Lampard amesema kuwa wachezaji wake walionekana wamechoka kwenye mchezo huo jambo lililowafanya washindwe kuibuka na ushindi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako