• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Yanga inashuka dimbani kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya KMKM Dar

  (GMT+08:00) 2020-09-30 19:17:25

  Klabu ya Yanga leo inacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya KMKM ya Zanzibar, mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Azam Complex. Mchezo huo wa leo ni maalumu kwa ajili ya kujiweka sawa na mechi za Ligi Kuu Bara zinazoendelea ambapo kwa sasa ligi inaingia mzunguko wa tano. Katika mchezo wa Yanga kwa mzunguko wa tano itakutana na Coastal Union ya Juma Mgunda katika uwanja Uwanja wa Mkapa, Oktoba 3 unatarajiwa kupigwa majira ya saa 1:00 usiku. Yanga mechi yao iliyopita ndani ya ligi wametoka kushinda bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri Morogoro wanakutana na Coastal Union iliyotoka kushinda bao 1-0 mbele ya JKT Tanzania. Hii inakuwa ni mechi ya pili ya kimafiki kwa Yanga kucheza ndani ya Uwanja wa Azam Complex ambapo kabla ya kuvaana na Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba ilimenyana na Mlandege ya Zanzibar. Kwenye mchezo huo Yanga ilishinda mabao 2-0 ambapo yalifungwa na Wazir Junior na Tonombe Mukoko.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako