• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwenyekiti wa TFF Bw Wallace Karia atangaza neema Mkwakwani

  (GMT+08:00) 2020-09-30 19:17:52

  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limetangaza kuandaa mchakato wa kuujenga upya Uwanja wa CCM Mkwakwani uliopo jijini, Tanga ili kufikia vigezo vya kimataifa. Rais wa TFF, Wallace Karia, alisema hayo juzi wakati akizungumza na wadau wa soka wa mkoa wa Tanga akiwamo Mkurugenzi wa Hoteli ya Tanga Beach Resort, Hamisi Kindoroko na Katibu wa CCM (Muheza), Mohamed Moyo. Karia alisema tayari ameshazungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella na wadau wengine ili kuanza maandalizi ya ukarabati wa uwanja huo ambao utasaidia kuinua kiwango cha wachezaji wa Tanga. Alisema sasa hivi wanatarajia kufanya mazungumzo na uongozi wa CCM Mkoa wa Tanga ili kupata ridhaa ya kuanza mchakato huo kwa sababu wao ndio wamiliki wa uwanja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako