• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Victor Wanyama asema atafanya kila analoweza kuisaidia Harambee Stars iende Qatar 2022

  (GMT+08:00) 2020-09-30 19:21:57

  Baada ya kuiongoza Kenya kushiriki fainali za Kombe la Afrika (AFCON) nchini Misri kwa mara ya kwanza tangu 2004, kiungo na nahodha wa Harambee Stars Victor Wanyama sasa ana malengo mapya ndani ya jezi za timu ya taifa Kenya. Nyota huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur amesema hana nia ya kutundika daruga zake katika soka ya kimataifa hivi karibuni, na kubwa zaidi katika maazimio yake ni kuongoza Kenya kushiriki fainali za Kombe la Dunia za 2022 nchini Qatar. Lakini haitakuwa kazi rahisi kufanya hivyo kwani Harambee Stars italazimika kuwafunga Mali, Uganda na Rwanda na kuibuka kileleni mwa Kundi E katika safari yao ya kujikatia tiketi ya kutua Qatar. Wanyama amesema wapo kwenye kundi gumu na wanaheshimu kila kikosi, lakini badala ya kuongopa timu nyingine wanatakiwa kujifua vilivyo na kuwabwaga kwa sababu hakuna lisilowezekana katika soka

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako