• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya China yafanya hafla ya maadhimisho ya siku ya taifa

    (GMT+08:00) 2020-09-30 20:49:40

    Baraza la serikali la China leo usiku limefanya hafla ya siku ya taifa ya kuadhimisha miaka 71 tangu kuanzishwa kwa China. Rais Xi Jinping wa China, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang, viongozi wengine wa chama na serikali pamoja na watu karibu 500 wa China na nchi za nje wamehudhuria hafla hiyo.

    Bw. Li Keqiang amesema huu ni mwaka usio wa kawaida katika historia ya Jamhuri ya watu wa China. Kutokana na kukabiliwa changamoto kubwa za maambukizi ya virusi vya Corona na kudidimia kwa uchumi wa dunia, China inaratibu kuhimiza kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya Corona na maendeleo ya uchumi na jamii, kupata mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona, kutimiza ongezeko la uchumi na kupata mafanikio ya kupunguza umaskini, maisha ya watu wa China yamepata uhakikisho mkubwa.

    Amesema China inapaswa kushikilia imani, kukabiliana na changamoto, na kutilia mkazo katika mambo yake. Inapaswa kushikilia kufanya mageuzi kwa kina, kuhimiza kufungua mlango kwa kiwango cha juu. Kote nchini inapaswa kujitahidi kutimiza malengo makuu ya mwaka huu na kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako