• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu Mkuu wa UM atoa wito wa kuwa na azma kubwa ya kurejesha uanuai wa viumbe uliopotea

    (GMT+08:00) 2020-10-01 09:13:44

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kuwepo kwa azma kubwa ya kurejesha uanuai wa viumbe uliopotea.

    Akiongea kwenye Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Mataifa kuhusu anuai ya viumbe, Bw. Guterres amesema uanuai wa viumbe na mfumo wa ikolojia ni muhimu kwa maendeleo na ustawi wa binadamu na pia ni muhimu katika kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu na utekelezaji wa makubaliano ya Paris ya mabadiliko ya tabia nchi.

    Aidha ametaja vipaumbele vitatu vya uhifadhi na usimamizi endelevu wa uanuai wa viumbe, vikiwemo ufumbuzi unaohusu maumbile unapaswa kuingizwa wakati nchi zikifufuka kutokana na janga la COVID-19 na mipango mipana ya maendeleo, mifumo ya uchumi na masoko ya fedha ni lazima ihesabiwe katika uwekezaji wa maumbile na pia kusema kuna umuhimu wa kuweka sera nzuri zaidi na malengo ambayo yatalinda anuai ya viumbe na kutomwacha yeyote nyuma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako