• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM wakaribisha dola za kimarekani bilioni moja zilizoahidiwa kutolewa ili kumaliza janga la virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-10-01 09:34:08

    Umoja wa Mataifa na washirika wake jana Jumatano ulikaribisha "ishara muhimu ya mshikamano" baada ya serikali, sekta binafsi, vyama vya kiraia na mashirika ya kimataifa kuahidi kuunga mkono Pendekezo la Kuharakisha Upatikanaji wa Nyenzo za Kukabiliana na COVID-19 lililotolewa na Shirika la Afya Duniani WHO pamoja na washirika wa kimataifa.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa, karibu dola za kimarekani bilioni moja zimeahidiwa kutolewa kwa ajili ya pendekezo hilo, ambalo ni mpango mkubwa zaidi wa pande nyingi unaolenga kumaliza janga la virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako