• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tunisia na Marekani zajadiliana kuhusu masuala ya kupambana na ugaidi na mgogoro wa Libya

    (GMT+08:00) 2020-10-01 17:48:33

    Rais Kais Saied wa Tunisia na waziri wa ulinzi wa Marekani Bw. Mark Esper ambaye yupo nchini Tunisia kwa ziara, wamejadiliana kuhusu ushirikiano kwenye mapambano dhidi ya ugaidi na mgogoro wa Libya.

    Kwa mujibu wa shirika la habari la Tunisia, Rais Saied amesema mgogoro wa Libya unapaswa kutatuliwa na pande husika za ndani za Libya bila uingiliaji wa nguvu ya nje. Ikiwa ni nchi jirani wa Libya, Tunisia inaunga mkono utatuzi wa kisiasa wa suala hilo ili kuhakikisha mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya Libya.

    Bw. Esper amesema Marekani pia inatarajia mgogoro wa Libya utatatliwa kwa amani ili kutimiza utulivu wa kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako