• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Walinzi amani wa China nchini Lebanon wachangia ukarabati mjini Beirut

    (GMT+08:00) 2020-10-01 18:16:30

    Baada ya maandalizi ya siku tatu, kikundi cha 19 cha kikosi cha uhandisi cha kulinda amani cha China nchini Lebanon jana kiliingia kwenye eneo la mlipuko wa bandari ya Beirut na mitaa ya mji huo, kushiriki rasmi kwenye kazi ya ukarabati mjini humo.

    Naibu kamanda wa kikosi hicho Xiong Chaochun, amesema hivi sasa maafisa na wanajeshi wa China wanashughulikia jukumu la ukarabati wa eneo la bandari ya Beirut na mitaa mjini humo, na wamegawanywa katika vikundi viwili kufanya kazi kwa wakati mmoja. Pia ameeleza kuwa jukumu hilo ni gumu tena ni hatari, kwani mbali na ugumu wa kuondoa kifusi cha mlipuko, bado kuna kemikali hatari zisizojulikana kwenye eneo la tukio, na mapaa ya majengo mjini humo pia yameharibiwa vibaya. Zaidi ya hayo, wanajeshi hao wanakabiliwa na hatari ya janga la virusi vya Corona.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako