• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Seneti Marekani lapitisha mswada wa muda wa matumizi ili kuepusha kufungwa kwa serikali

    (GMT+08:00) 2020-10-01 18:17:58

    Baraza la seneti la Marekani limepitisha mswada wa muda wa matumizi ili kuipatia fedha serikali kuu hadi mwezi Desemba, saa chache kabla ya mswada wa matumizi kwa mwaka mzima kukaribia kwisha na serikali kukaribia kufungwa.

    Mswada huu umepitishwa kwa kura 84 za ndio na kumi za hapana, baada ya kupitishwa na baraza la wawakilishi wiki iliyopita. Rais Donald Trump anatarajiwa kusaini mswada huo ili kuepusha serikali kukosa fedha kabla ya uchaguzi mkuu.

    Spika wa baraza la wawakilishi Bibi Nancy Pelosi alifikia makubaliano na waziri wa fedha wa Marekani na wawakilishi wa chama cha Republican kuhusu mswada wenye dola bilioni 8 za msaada wa chakula na dola bilioni 21 za msaada kwa wakulima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako