• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa China katika UN: Hotuba ya Rais Xi kuhusu uhifadhi wa viumbe anuawai inaipa jumuiya ya kimataifa mwangaza na matumaini

    (GMT+08:00) 2020-10-01 18:18:28

    Balozi wa China katika Umoja wa Mataifa Zhang Jun amesema, kutokana na uwepo wa hali mbaya ya mabadiliko ya tabianchi, kuenea kwa virusi vya Corona na kudidimia kwa uchumi, dunia imejaa hisia za wasiwasi na huzuni, lakini hotuba aliyotoa Rais Xi Jinping wa China katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhifadhi wa viumbe anuawai inaipa jumuiya ya kimataifa mwangaza na matumaini.

    Kwenye hotuba hiyo iliyotolewa jana kwa njia ya video, Rais Xi amesisitiza umuhimu wa kushirikisha nguvu za nchi zote ili kukabiliana na changamoto kwa mazingira ya dunia. Balozi Zhang amesema, "Pamoja Tunaweza." Msimamo wa China ni tofauti kabisa na nchi chache zinayokataa kutekeleza wajibu na majukumu ya kimataifa.

    Balozi Zhang aliongeza kuwa, uhifadhi wa viumbe anuwai ni suala linalohusu kwa karibu maendeleo endelevu ya binadamu, ndiyo maana ni moja ya changamoto kubwa zinazoikabili dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako