• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Pigo kwa Harambee Stars Baada ya Wanyama na Omollo kujitoa kikosini

  (GMT+08:00) 2020-10-01 19:10:45

  Baada ya kukosa huduma za mshambuliaji Michael Olunga wa Kashiwa Reysol ya Japan katika jumla ya mechi nne zijazo, timu ya taifa ya Harambee Stars imepatwa na pigo jingine baada ya uwezekano wa kumpata nahodha wake Victor Wanyama na kiungo Johanna Omollo umekuwa mgumu kutokana na mazingira ya sasa ya virusi vya Corona duniani, na wachezaji hao hawatakuwa sehemu ya mechi nne zijazo za kutafuta nafasi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Afrika (AFCON) 2021. Kutokana na masharti makali yanayodhibiti kuenea kwa virusi vya corona katika mataifa wanakocheza Wanyama na Omollo, Matumaini ya kuwasadikisha waajiri wao kuwaachilia yanazidi kudidimia," ikasema sehemu ya taarifa ya Shirikisho la Soka Kenya (FKF).

  Wanyama kwa sasa anachezea Montreal Impact ya Canada huku Omollo akisakatia Cercle Brugge nchini Ubelgiji. Harambee starts wamepangiwa kuvaana na Comoro katika mkondo wa kwanza jijini Nairobi Novemba 9 kabla ya kurudiana na kikosi hicho jijini Moroni siku nne baadaye.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako