• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Programu ya Teksi ya Ethiopia kuingiza Sh2bn katika sekta ya bodaboda nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2020-10-01 20:40:05

    Huduma ya kuita teksi mtandaoni kutoka Ethiopia inayoitwa Taxiye imeingia katika soko la Kenya ,kuongeza ushindani katika sekta hiyo.

    Afisa Mkuu Mtendaji wa Taxiye , Eve Maina,amesema kuwa watawekeza Sh2 bilioni katika biashara hiyo kwa kuwajumuisha waendeshaji bodaboda na madereva wa teksi ili kuwakodishia magari na pikipiki kwa ajili ya biashara.

    Maina alisema wanashirikiana na wahudumu wa teksi na bodaboda ili kuwapatia fursa ya kushiriki katika mchakato wa maamuzi wa kampuni hiyo kwa kuwakodishia pikipiki na magari kwa bei nzuri.

    Alisema kuwa kwa kiwango kidogo cha Sh250 kwa siku, wahudumu wa bodaboda wataweza kumiliki pikipiki zao na simu janja kwa ajili ya shughuli zao.

    Kampuni hiyo itashirikiana na Chama cha Wamiliki wa Bodaboda nchini Kenya (BAK) na inapanga kuwapatia wanachama pikipiki 300,000 katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

    Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Bodaboda (BAK) Kevin Mubadi alisema ushirikiano huo utatoa fursa nyingi zaidi katika sekta hiyo inayohudumia watu zaidi ya milioni 1.2.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako