• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yahimizwa kurahisisha harakati za malori kwenye mpaka wa Tanzania

    (GMT+08:00) 2020-10-01 20:40:43

    Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) linataka watu wote wanaoingia Kenya kutokea Tanzania kutendewa sawa ,bila kujali kama ni madereva wa malori au wananchi wa kawaida.

    Hivi sasa,wananchi wa kawaida kutoka Tanzania wanaruhusiwa kuendelea na safari wanapotoa cheti cha Covid-19.

    Hata hivyo madereva wa malori wanahitajika kutoa cheti cha Covid-19 kutoka Tanzania nab ado wanapimwa tena katika kituo cha mpaka na wanaruhusiwa kuingia Kenya majibu ya vipimo vyao kutoka.

    Kulingana na maafisa wa uhamiaji wa Tanzania ,mchakato huo unachukua zaidi ya wiki ,hatimaye kuchelewesha uwasilishaji wa bidhaa.

    Afisa Mkuu Mtendaji wa EABC Peter Mathuki pia ametoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa umma na binafsi kati ya Kenya na Tanzania ili kuboresha biashara baina ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako