• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zanzibar-Wateja wa mtandao wa Zantel sasa wanaweza kulipia bili za maji kupitia Ezypesa

    (GMT+08:00) 2020-10-01 20:40:58

    Wateja wa mtandao wa simu wa Zantel sasa wanaweza kulipia bili za maji kiurahisi zaidi kwa njia ya Ezypesa baada ya kampuni hiyo kuingia ubia na Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), mfumo wa kidigitali zaidi wa kufanya malipo.

    Hatua hiyo itaongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato huku ikiwapunguzia wateja adha ya kusafiri umbali mrefu, ili kulipia huduma hiyo muhimu.

    Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (Zawa) , Mussa Ramadhan, alipongeza hatua hiyo akieleza kuwa, itasaida katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja visiwani Zanzibar..

    Ramadhani alisema huduma hiyo ni suluhisho katika kuongeza kasi na ufanisi wa ukusanyaji wa mapato hivyo kusaidia mamlaka kuwa na uwezo wa kuboresha miundombinu ya maji na kuwafikia watu wengi zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako