• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamishna wa Haki za Binadamu wa UM asema wanaendelea kupokea ripoti za ubaguzi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika.

    (GMT+08:00) 2020-10-02 08:49:50

    Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Matifa Michelle Bachelet jana alitoa taarifa mpya juu ya ubaguzi wa kimfumo kwenye mkutano wa 45 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, akisema ofisi yake inaendelea kupokea ripoti za ukatili na ubaguzi wa polisi dhidi ya watu wenye asili ya Afrika.

    Pia ameripoti kwenye baraza hilo shughuli zake ndani ya utaratibu wa Mwongo wa Kimataifa kwa Watu wenye Asili ya Afrika, akisema kutokuwepo kwa usawa wa kimuundo na ubaguzi wa rangi kumesababisha vurugu dhidi ya watu wenye asili ya Afrika zinazofanywa na polisi.

    Aidha amesema ukali na ubaya wa janga la COVID-19 kwa watu wenye asili ya Afrika pia umefichua kutengwa kwao. Hivyo amesema kumalizwa kwa matendo haya pamoja na mengine yanayoumiza ambayo yanasababishwa na ubaguzi wa rangi uliokita mizizi kwenye taasisi mbalimbali ni muhimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako