• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping ahutubia mkutano wa Baraza Kuu la UM kuhusu mambo ya wanawake

    (GMT+08:00) 2020-10-02 08:58:30

    Rais Xi Jinping wa China amehutubia mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuadhimisha miaka 25 tangu kufanyika kwa Mkutano wa Wanawake Duniani wa Beijing kwa njia ya mtandao, akipendekeza kutekeleza kihalisi usawa wa kijinsia, na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mambo ya wanawake.

    Rais Xi amesisitiza kuwa katika miaka 15 iliyopita, moyo wa mkutano wa wanawake duniani wa Beijing umeleta mabadiliko chanya, na wadhifa wa wanawake duniani umeimarika zaidi. Ametoa mapendekezo manne ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wanawake kuondoa taabu iliyosababishwa na janga la COVID-19, kutekeleza kihalisi usawa wa kijinsia, kuwahimiza wanawake wawe mbele zaidi katika maendeleo ya kizama, na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika mambo ya wanawake.

    Amesema kuhakikisha usawa wa kijinsia ni sera ya kimsingi ya China, ambayo imejenga mfumo wa zaidi ya sheria 100 za kulinda haki za wanawake. Ameongeza kuwa China pia imeondoa pengo la kielimu kati ya wanawake na wanaume, na wanawake wenye ajira wanachukua zaidi ya asilimia 40 ya watu wenye ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako