• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China aona hotuba za rais Xi Jinping zimeonesha mtizamo wa dunia na uwajibikaji wa nchi kubwa

    (GMT+08:00) 2020-10-02 16:51:49

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo amefahamisha hali kuhusu rais Xi Jinping kushiriki Mikutano ya ngazi ya juu ya Maadhimisho ya Miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa.

    Bw. Wang amesema hotuba muhimu alizozitoa rais Xi zimejibu maswali makuu juu ya binadamu watakabiliwa dunia ya aina gani baada ya janga la COVID-19, China itatoa mchango gani kwa dunia, pia zimesisitiza kanuni za kimsingi za China, kwamba inafuata uratibu wa pande nyingi kwa hatua madhubuti, kulinda mamlaka na ushawishi wa Umoja wa Mataifa, kufuata njia ya kujiendeleza kwa amani, kupata maendeleo ya kunufaishana, na kukuza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

    Anaona hotuba hizo zimeingiza msukumo mpya katika ushirikiano wa mapambano dhidi ya COVID-19 duniani, kupata maafikiano mapya kuhusu mageuzi ya mfumo wa utawala wa dunia; kutoa mapendekezo mapya kuhusu kuhimiza ufufukaji wa uchumi duniani, kuweka malengo mapya ya ujenzi wa ustaarabu wa ikolojia wa dunia; kuongeza msaada kwa mambo ya wanawake duniani, na kuonesha uwajibikaji katika kuunga mkono uongozi wa Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako