• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Dr Tedros atoa wito tena wa mshikamano wa nchi zote katika kukabiliana na virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-10-02 16:55:12

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la afya duniani WHO Dr Tedros Ghebreyesus kwa mara nyingine amesisitiza umuhimu wa mshikamano wa nchi zote katika juhudi za kumaliza kuenea kwa virusi vya Corona duniani. Akihutubia mkutano wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Dr Tedros alisema wanasayansi wanajitahidi kutoa mbinu mpya za upimaji, tiba na chanjo, hata hivyo cha muhimu zaidi ni mshikamano. Bila mshikamano, sayansi na mbinu hizo hazitafanya kazi.

    Katika mkutano huo wa kujadili mradi wa kuharakisha upatikanaji wa mbinu za kukabiliana na COVID-19,Dr Tedros alisema mradi huo umepata maendeleo mazuri, na kutokana na makubaliano yaliyofikiwa hivi karibuni kati ya WHO na washirika, nchi zenye pato la chini na wastani zitapata vifaa milioni 120 vya upimaji. Lakini bado kuna upungufu wa dola za kimarekani bilioni 35. Aliongeza kuwa pamoja na ufadhili wa kutosha, mradi huo utasaidia kudhibiti kuenea kwa virusi vya Corona, kurejesha imani ya watu na kuchochea ufufuaji wa uchumi. Dr Tedros alisisitiza kuwa sasa ni wakati wa kutambua utu tulio nao.

    Mradi huo uliozinduliwa Aprili 24 na Shirika la WHO unalenga kuharakisha utafiti na uzalishaji wa chanjo, vifaa vya upimaji na tiba vinavyohusu COVID-19, na kugawanya vifaa hivyo kwa haki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako