• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yashuhudia watalii karibu milioni 100 wa ndani katika siku ya kwanza ya mapumziko ya siku ya taifa

    (GMT+08:00) 2020-10-02 16:59:58

    Takwimu kutoka wizara ya utamaduni na utalii ya China imesema, katika siku ya kwanza ya mapumziko ya siku ya taifa inayoambatana na sikukuu ya Mwezi ambayo ni sikukuu ya jadi, China imeshuhudia watalii milioni 97 wa ndani na kuingiza dola za Marekani bilioni 11.3 kutokana na utalii.

    Takwimu zinaonesha kuwa, kwa jumla hali ya mawasiliano na usafiri kote nchini iko shwari, na matumizi ya barabara kuu yameongezeka. Hadi kufikia jana saa sita mchana, idadi ya magari yaliyotumia barabara kuu nchini China iliongezeka kwa asilimia 87.17 ikilinganishwa na siku iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako