• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TOSCI yatoa onyo kali kwa wauzaji na wasambaza mbegu Tanzania

    (GMT+08:00) 2020-10-02 19:08:38

    Taasisi ya Udhibiti wa Mbegu nchini (TOSCI), imetahadharisha kampuni zinazouza na kusambaza mbegu kuacha kuwauzia wakulima mbegu feki ili kuzuia hasara kwa wananchi.

    Mkaguzi wa mbegu kutoka TOSCI Makao Makuu jijini Dodoma, Dk. Mngotosha Ngomuo, alitoa tahadhari hiyo wakati maofisa wa taasisi hiyo kutoka makao makuu pamoja na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini walipofanya ukaguzi wa kawaida wa mbegu kwenye maduka mbalimbali yanayouza pembejeo.

    Alisema mfanyabiashara atakayekamatwa anasambaza mbegu hizo atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani kwa maelezo kuwa vitendo hivyo vinafifisha juhudi za serikali za kuinua kilimo.

    Alizitaja mbegu ambazo zinatafsiriwa ni feki ni ambazo hazijakaguliwa na mamlaka hiyo na kuwekwa nembo, zilizopitwa na muda wake pamoja na zinazoingia nchini humo kupitia njia za panya kutoka mataifa mengine. Alisema kwenye ukaguzi huo walibaini mbegu nyingi zinazouzwa kwenye maduka zimepitwa na wakati na hivyo wakaziondoa ili wafanyabiashara hao wasiendelee kuzisambaza.

    Alisema usambazaji wa mbegu feki una madhara makubwa kwa wakulima ikiwemo kuwasababishia wakulima hasara ya kutovuna kabisa mazao kama ambavyo wanakuwa wamekusudia.

    Aliwataka wauzaji wa mbegu hizo kuwa wazalendo kwa kuhakikisha wanaepuka kusambaza mbegu hizo huku akidai kuwa wao ni wasimamizi wa sheria na hawapendi kuwachukulia hata wafanyabiashara na ndiyo maana wanatoa elimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako