• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha wa Arsenal asema aridhishwa na uwezo wa golikipa wake

    (GMT+08:00) 2020-10-02 19:14:59

    MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa golikipa wake namba moja Bernd Leno alionyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo wa Carabao Cup uliochezwa usiku wa kuamkia leo dhidi ya Liverpool. Mchezo huo wa raundi ya 16 uliopigwa katika Uwanja wa Anfield, dakika 90 zilikamilika bila kufungana na kupelekea kupigwa mikwaju ya penalti ambapo Arsenal ilishinda kwa penalti 5 -4 za Liverpool. Ushindi huo unakuwa wa pili kwa Arsenal kuishinda Liverpool kwa penalti baada ya mwezi mmoja kupita kwani ilisepa na taji la Ngao ya Jamii mwezi Agosti kwa ushindi wa Penalti 5-4. Arteta amesema wana magolikipa wawili wazuri na wanaofanya kazi kwa umakini, jambo ambalo linampa matumaini ya kufanya vizuri hatua inayofuata ambayo ni robo fainali na watakapokutana na Manchester City.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako