• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Yanga yapiga hesabu ya kupata pointi tatu toka kwa Coastal Union kesho

    (GMT+08:00) 2020-10-02 19:15:18

    Wakati kikosi cha Yanga kikizidi kulalamikiwa na mashabiki wake kwa kushindwa kuonyesha soka la kuvutia, huku kila mchezaji akibaki kucheza kwa uwezo wake binafsi uwanjani, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Juma Mwambusi amesema mechi za kirafiki wanazocheza zinawasaidia kupata mwanga wa aina ya wachezaji wapya. Yanga juzi usiku iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMKM ya Zanzibar katika mechi ya kirafiki iliyopigwa Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, ikiwa ni maandalizi ya kuikabili Coastal Union kesho katika Uwanja wa Mkapa. Mwambusi amesema wachezaji wao ni wazuri na wana uwezo mkubwa, lakini wanahitaji kupata wachezaji ambao wanaweza kupambana kulingana na mpinzani wao wanayetarajia kukutana naye katika ligi hiyo. Alisema mbali na kupata mwanga huo, lakini wanatengeneza ushindani mkubwa wa wachezaji wao kuhakikisha wanapata namba katika kikosi cha kwanza na kusaidia kupata matokeo chanya kwa kila mechi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako