• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ratiba ya Kombe la Klabu Bingwa Ulaya yatajwa, Manchester United yawekwa kundi gumu

    (GMT+08:00) 2020-10-02 19:15:35

    Kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer kimewekwa Kundi H pamoja na wana fainali Paris Saint-Germain ya Ufaransa, RB Leipzig ya Ujerumani na Istanbul Basaksehir ya Uturuki ikiwa ni safari ya kutafuta kombe hilo kwa mwaka kesho. Kundi A linazikutanisha bingwa mtetezi, Bayern Munich ya Ujerumani, Atletico Madrid ya Hispania, RB Salzburg ya Ujerumani na Lokomotiv Moscow ya Russia. Kundi B kuna Real Madrid ya Hispania, Shakhtar Donetsk ya Uturuki, Inter Milan ya Italia na Borussia Monchengladbach ya Ujerumani. Kundi C; Porto ya Ureno, Manchester City ya England, Olympiacos ya Ugiriki na Marseille ya Ufaransa. Kundi D kuna Liverpool ya England, Ajax ya Uholanzi, Atalanta ya Italia na Midtjylland ya Denmark. Kundi E kuna Sevilla ya Hispania, Chelsea ya England, Krasnodar ya Urusi na Rennes ya Ufaransa. Fainali ya msimu huu itafanyika Mei 29, mwakani Uwanja wa Ataturk Jijini Istanbul, ambako Liverpool ilifanya maajabu ya kutosahaulika baada ya kutoka nyuma kwa 3-0 na kuifunga AC Milan kwa penalti mwaka 2005.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako